Inter Milan wanusa taji la kwanza la Serie A baada ya miaka 11 kwa ushindi mwembamba dhidi ya Bologna

Inter Milan wamekwea kileleni kwa tofauti ya alama nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A kufuatia kuwachapa bao 1-0 Bologna mtanange uliopigwa Jana Jumamosi Aprili 3.

Lukaku aliipa uongozi Inter kunako dakika ya 31 ya mchezo ungwe ya kwanza kwa kichwa ambacho kilimshinda mlinda mlango Federico Ravaglia.

Bologna walishindwa kutoa upinzani mkubwa katika mechi ambayo  mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez aligongesha mwamba dakika ya 50 kwa upande wa Inter.

Ushindi unampa kocha Antonio Conte matumaini ya ubingwa wa kwanza tangia mwaka 2009/10.

Kwingineko, wapinzani wa karibu AC Milan walibanwa na Sampdoria Jumamosi kwa sare ya 1 – 1

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares