Inter Milan washinda Dabi ya Milan na kuongoza msimamo wa Serie A kwa kuichapa AC Milan 3-0

Inter Milan imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya wapinzani wao wa karibu AC Milan katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia uliopigwa Leo Jumapili na kukwea mpaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Serie A.

Magoli mawili ya Lautaro Martinez yaliwapa auheni Inter mbele ya AC Milan ambao wameongoza msimamo wa Ligi kwa muda mrefu huku wakiwa kwenye kiwango bora.

Staa Zlatan Ibrahimovic alikuwa aipatie timu yake magoli mawili lakini haikutokea hivyo kabla ya Romelu Lukaku kufunga goli la tatu na kumaliza kabisa mchezo, goli la Lukaku linamfanya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga goli katika mechi nne mfululizo za Dabi ya Milan tangia Benito Lorenzi alipofanya hivyo mwaka 1950.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares