Inter Milan Yatinga Nusu Fainali, Benfica nje

124

Inter Milan imetoa sare ya bao 3-3 na Benfica katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufuzu nusu fainali kwa kutumia matokeo chanya ya mchezo wa kwanza ambapo walishinda bao 2-0.

Matokeo ya kufuzu yanafanya Inter Milan sasa watakutana na wapinzani wa karibu kwenye Ligi Kuu ya Italia Serie A kwa mara ya kwanza tangia mwaka 2005.

Kwenye mechi iliyochezwa uwanjani San Siro, mabao ya Inter Milan yamefungwa na Nicolo Barella, mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez na Joaquin Correa wakati mabao matatu ya wageni Benfica yakiwekwa kimiani na Fredrik Aursnes Antonio Silva na Petar Musa.

Author: Asifiwe Mbembela