Inter, Roma, Milan mawindoni nafasi za Champions League

46

Nchini Italia mapambano yatakuwa makali katika mechi za katikati ya wiki hii, wakati timu zaba zikitafuta pointi muhimu za kucheza kandanda la Ulaya katika sehemu ya mwisho ya msimu uliotawaliwa na mabingwa watarajiwa Juventus.

Inter Milan, AC Milan na Roma zinalenga kujinyanyua baada ya vichapo vya wikendi katika Serie A. huku zikiwa zimesalia mechi tisa, Inter wako nafasi ya tatu baada ya kufungwa 1 – 0 Jumapili na Lazio, wakati AC Milan ambao walifungwa pia 1 -0 na Sampdoria wakiwa nyuma yao na pengo la pointi mbili na wanajaza nafasi ya nne na ya mwisho ya Champions League

Roma wakati huo huo wameanguka hadi nafasi ya saba baada ya kubamizwa 4 – 1 nyumbani dhidi ya Napoli. Milan watakwaruzana kesho Jumanne na Udinese. Vinara Juve watacheza dhidi ya Cagliari, huku nambari mbili Napoli ambao wana mwanya wa pointi 15 wakicheza dhidi ya Empoli. Roma watacheza Jumatano dhidi ya Fiorentina

Author: Bruce Amani