Inter yajiweka sawa ubingwa wa Serie A, yatoa kipondo kwa Crotone

Inter Milan wameendelea kuukaribia zaidi ubingwa wa Ligi Kuu nchini Italia kufuatia kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Crotone huku Christian Eriksen na Achraf Hakimi wakifunga goli kila mmoja.

Inter wanaweza kutawazwa kuwa mabingwa endapo timu ya Atalanta itashindwa kuvuna alama tatu mbele ya Sassuolo mwendelezo wa mbilinge mbilinge za Serie  A.

Kiungo mshambuliaji wa Denmark Eriksen alifunga goli la kwanza dakika chache baada ya kuingia akitokea benchi kabla ya Hakimi kufunga bao la pili na dakika za lala salama, kipigo hicho kinaifanya Crotone kushuka daraja baada ya msimu mmoja.

Hata kama Atalanta atashinda dhidi ya Sassuolo, bado ubingwa kwa inter Milan ni ngumu kuuzuia kutokana na kuhitaji alama moja kwenye mechi nne zilizosalia kutwaa taji la Scudetto.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares