Italia yatoa kichapo kizito kwa Czech wakati ikipasha misuli kuelekea Euro 2020

Timu ya Taifa ya Italia imeipiga 4-0 Jamhuri ya Czech katika mchezo wa maandalizi kuelekea michuano ya Euro 2020, mtanange uliopigwa Bologna Ijumaa Mei 4.
Mshambuliaji Ciro Immobile alifunga goli la kwanza na la 13 katika majukumu ya timu yake ya taifa, Nicolo Barella aliingia kambani bao la pili, akisherekea kuzaliwa kwake miaka 30, Lorenzo Insigne alifunga goli la tatu akimalizia pasi ya immobile.
Bao la nne limefungwa na Domenico Berardi akitumia vyema pasi ya Lorenzo.
Unakuwa mchezo wa nane mfululizo kwa Italia kwenye mashindano yote kucheza bila kupoteza wala kuruhusu goli.
Kuelekea Euro 2020, Italia imepangwa kundi A na timu ya Wales, Switzerland. Kundi la Czech ipo kundi D na England, Croatia na Scotland.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares