James ampisha Ronaldo Man United, atua Leeds United

Leeds imemsajili winga wa Manchester United Daniel James kwa kiasi cha fedha takribani pauni milioni 25, baada ya kutumika Man United kwa miaka miwili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amemwaga wino wa miaka mitano katika klabu inayonolewa na kocha Marcelo Bielsa.

Leeds ambao wamekuwa wakivutiwa kumsajili James kwa muda mrefu sasa wametimiza matakwa yao huku ujio wa staa Cristiano Ronaldo ukitajwa pia sababu iliyopelekea winga huyo wa Wales kuondoka viunga vya Old Trafford.

“Naamini nimefanya maamuzi sahihi kwa minajili ya taaluma yangu ya soka”, alisema James.

Katika mechi 74 alizocheza kwa Mashetani Wekundu, Daniel James amefunga goli 9 pekee ambapo mechi ya mwisho ilikuwa dhidi ya Wolves ambapo Manchester United walishinda bao 1-0.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares