Jamii nzima ya Leicester City yaomboleza

Mke na mtoto wa kiume wa mmiliki wa Leicester City wameweka shada la maua katika uwanja wa King Power baada ya mfanyabiashara huyo kufariki dunia pamoja na watu wengine wanne katika ajali helikopta iliyokuwa imewabeba.

Katika ajali hiyo Vichai Srivaddhanaprabha, maafisa wawili wa timu, rubani, na abiria mmoja wote walikufa wakati ndege hiyo ilipopoteza mwelekeo na kuanguka nje ya uwanja huo katika eneo la kuegesha magari.

Kikosi cha kwanza cha timu hiyo na timu ya vijana pia walifika katika uwanja wa King Power kutoa heshima zao.

Timu inayochunguza ajali hiyo ya Jumamosi usiku imepata vifaa vya dijitali vya kunasa mawasiliano ya rubani

Kikosi cha jeshi la polisi cha Leicester kimetaja watu wengine waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Nursara Suknamai, Kaveporn Punpare, nahodha Eric Swaffer na mpenzi wake Izabela Roza Lechowicz.

Mke wa Mwenyekiti wa klabu hiyo Aimon na mtoto wake wa kiume Aiyawatt Srivaddhanaprabha waliungana uwanjani na Rais wa shirikisho la kandanda la Thailand Somyot Poompanmoung pamoja na mke wake Potjaman Poompanmoung katika maombolezo hayo.

Kocha Claude Puel pia aliungana na wachezaji katika kuomboleza. Watu maarufu kwenye michezo na wachekeshaji nao walikuwa sehemu ya waliohudhuria tukio hilo lilofanyika katika uwanja wa King Power.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends