Japan mabingwa wa dunia wa kandanda kwa wanawake

Japan ndio mabingwa wapya wa kombe la dunia kwa wanawake wasiozidi miaka 20. Akina dada kutoka Japan walinyakua taji hilo, baada ya kuilaza Uhispani mabao 3-1 katika fainali iliyochezwa jana katika uwanja wa Stade de la Rabine, nchini Ufaransa.

Bara la Afrika liliwakilishwa na Nigeria na Ghana. Ghana iliyondolewa katika hatua ya makundi, huku Nigeria ikiondolewa katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Uhispania mabao 2-1.

Makala ya 10, ya fainali hii itakuwa mwaka 2020.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends