Je, ni msimu wa Liverpool kutoroka na ubingwa wa ligi?

Wengi waliusubri kwa hamu mchuano huo. Na baada ya matanange huo, inakuwa ni vigumu kwa kutoamini kuwa vijana wa kocha Jurge Klopp ndio watakaotoroka na kombe la ligi msimu huu. Ilikuwa mechi kati ya bingwa wa Ulaya na bingwa wa ligi.

Lakini je, itakapofika Mei mwaka ujao, bingwa wa Ulaya ndiye atakayekuwa tena bigwa wa ligi? Liverpool waliwashinda Manchester City ya Pep Guardiola 3 –1 uwanjani Anfield kwenye mechi iliyojaa vituko, vikiwemo vya maamuzi ya VAR na mambo kama hayo.

Ni matokeo yanayoonyesha ujasiri na matumaini ya Liverpool kwamba baada ya kukosa ubingwa wa msimu uliopita kwa karibu mno, sasa mambo huenda yakawa mazuri msimu huu. Huenda wakabeba ubingwa wa ligi baada ya kusubiri kwa miaka 30

Liverpool sasa wanaongoza ligi na mwanya wa point inane mbele ya Leicester City na Chelsea, na pointi tisa mbele ya City. Kama Liverpool hawatabeba ubingwa wa msimu huu, watajilaumu wenyewe.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends