Jeshi la Algeria litakalopambana katika Afcon

Kocha wa timu ya taifa ya Algeria Djamel Belmadi amekitaja kikosi cha wachezaji 23 kuelekea fainali ya AFCON nchini Misri.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Riyad Mahrez anayecheza katika klabu ya Manchester City ya Uingereza.

Hata hivyo, wachezaji wengine kama Faouzi Ghoulam, Nabil Bentaleb, wameachwa katika kikosi hicho.

Hata hivyo, Islam Slimani amejumuishwa katika kikosi hicho licha ya kufunga bao moja tu katika klabu yake ya Fenerbahce nchini Uturuki.

Algeria imepangwa pamoja na Kenya, Tanzania na Senal kuelekea katika michuano hiyo.

Kikosi kamili

Makipa: Rais M’Bolhi, Azzedine Doukha, Alexandre Oukidja

Mabeki : Ramy Bensebaini, Mohamed Fares, Youcef Atal, Mehdi Zeffane, Aissa Mandi, Djamel Benlamri, Rafik Halliche, Mehdi Tahrat

Viungo wa Kati: Mehdi Abeid, Hichem Boudaoui, Adlene Guedioura, Haris Belkebla, Ismael Bennacer, Sofiane Feghouli

Washambuliaji: Riyad Mahrez, Adam Ounas, Yacine Brahimi, Youcef Belaili, Baghdad Bounedjah, Islam Slimani

Author: Bruce Amani