Jesse Marsch atangazwa kuwa mrithi wa Nagelsmann katika klabu ya Leipzig

Kocha wa Red Bull Salzburg Jesse Marsch ataanza maisha mapya ya ukocha kwa kipindi cha miaka miwili kukinoa kikosi cha RB Leipzig akichukua nafasi ya Julian Nagelsmann mwishoni mwa msimu.

Marsch, 47, alikuwa kocha msaidizi ndani ya RB Leipzig msimu wa mwaka 2018/19, na anachukua mikoba ya Nagelsmann ambaye ametimukia Bayern Munich.

Akizungumzia juu ya ujio wa kocha mpya, Mkurugenzi wa Michezo klabuni hapo Oliver Mintzlaff amesema “Jesse anajua utamaduni wa uchezaji wetu, anajua filosofi yetu pia”.

Marsch amefanya kazi pia nchini Marekani katika klabu ya New York Red Bulls, nchini Austria alishinda taji la Ligi na mara Kombe la ndani.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares