Job Ajifunga Kuwatumikia Wananchi

314

Mlinzi wa kati wa kimataifa wa Tanzania Dickson Job ameongeza mkataba mpya wa kuitumikia kikosi cha Yanga, kandarasi ya miaka miwili.

Job, 22, ambaye amekuwa nahodha msaidizi klabuni hapo, mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni wa msimu huu na tetesi zilikuwa zimeanza za kumhusisha kuwa anatakiwa na klabu ya Simba na Azam FC.

Taarifa iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii ya Yanga imeeleza kuwa Job mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar atakuwa kwenye uzi wa timu ya wananchi kwa misimu miwili.

Author: Asifiwe Mbembela