Jorginho amfunika Kante, de Bruyne tuzo Uefa

55

Kiungo mkabaji wa Chelsea na Italia Jorginho ametajwa kama mchezaji bora wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa 2020/21.

Jorginho, 29, ametwaa tuzo hiyo akimshinda kiungo mwenza wa Chelsea na Ufaransa N’golo Kante pamoja na kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin de Bruyne.

Wakati huo huo, tuzo ya kocha bora imeenda kwa kocha Thomas Tuchel baada ya kukiongoza kikosi cha The Blues kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa upande wa Wanawake, nahodha wa Barcelona Alexia Putellas ameshinda tuzo wa mchezaji bora.

Tuzo za Uefa hutolewa na Shirikisho la Kandanda Ulaya ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi za wachezaji katika msimu husika wamashindano.

Author: Bruce Amani