Jose: Utd inaweza kuwa katika nne za kwanza ifikapo Januari

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa timu yake inaweza kuwa katika nafasi nne za kwanza katika Premier League ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba. United kwa sasa wako katika nafasi ya nane, pointi saba kutoka eneo la kufuzu katika Champions League.

Akizungumza kabla ya mchuano wa United na Crystal Palace Jumamosi, Jose mwenye umri wa miaka 55 amesema anafahamu kuwa pengo ni kubwa, lakini pia anafahamu kuwa  hadi mwishoni mwa Desemba watakuwa na mechi nane za kucheza kwenye ligi, na hiyo ina maana kuwa pointi 24.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends