Joshua Cheptegei avunja rekodi ya mbio za mita 10,000

Joshua Cheptegei amevunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 10, 000 wanaume. Cheptegei amevunja rekodi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Kenenisa Bekele wa Ethiopia kuanzia mwaka wa 2005 baada ya kukimbia kwa 26.11.00 na kuvunja rekodi ya Bekele ya muda wa 26.17.53.
Cheptegei ameiweka rekodi hiyo mpya katika mashindano ya NN Valencia yaliyoandaliwa katika uwanja wa Turia-Spain. Mwaka wa 2019, alivunja rekodi ya mbio za kilomita kumi za wanaume kwa kukimbia kwa dakika 26.38 lakini ikavunjwa tena mkenya Ronex Kipruto wa Kenya. Nchini Uganda ni wanariadha wawili tu ambao wamevunja na kuweka rekodi za dunia katika mashindano ya riadha.

Author: Bruce Amani