Juma Mgunda wa Coastal Union atoa mpango kabambe wa Ligi Kuu VPL

Kocha Mkuu wa Coastal Union Juma Mgunda amesema ameelekeza nguvu zote kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara mara baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya Shirikisho la Azam hatua ya 16 bora.
Coastal Union iliondolewa na Mwadui FC hatua ya 16 bora kwa kufungwa mabao 2-0 na kuwaacha wapinzani wao wakitinga hatua ya robo fainali, Uwanja wa Mwadui Complex.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mgunda amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zilizobaki ndani ya ligi ili waweze kusalia ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wa 2021/22.
Kwenye msimamo wa ligi, Coastal Union ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 28.
Katika hatua nyingine, Wagosi wa Kaya wamekanusha taarifa za kumfuta kazi Kocha Mgunda zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares