Junior Firpo wa Barcelona ajiunga na Leeds United

18

Leeds United imekamilisha uhamisho wa beki wa pembeni Junior Firpo kutokea Barcelona kwa dau la pauni milioni 13 kwa kandarasi ya miaka minne.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alitua viunga vya Camp Nou akitokea Real Betis mwaka 2019 na amecheza mechi 41 ambapo sasa amewekea kipengele cha asilimia 20 katika muuzo rasmi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Hispania katika umri wa miaka 21 aliisaidia Barcelona kushinda Copa del Rey msimu uliopita.

Author: Asifiwe Mbembela