Juve wapigwa, wakati Ronaldo aondoka kutua Man United

Juventus wamempoteza Ronaldo sawa na kukutana na kipigo cha goli 1-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Empoli katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A.

Matokeo hayo yanaifanya Juventus kushindwa kuibuka na ushindi kwenye mechi mbili za ufunguzi wa Ligi wakiwa na alama moja pekee. Itakumbukwa msimu uliopita pia walipoteza taji la Ligi likienda kwa Inter Milan.

Bao la Leonardo Mancuso ungwe ya kwanza lilitosha kabisa kuwapa ushindi Empoli dhidi ya Mabingwa hao wa Seria A mara 36.

Kipigo kinakuja ikiwa ni siku moja tangia klabu ya Manchester United kuthibitisha kuwa imefikia makubaliano ya kumsajili kwa mara nyingine staa Cristiano Ronaldo.

Juve walimaliza nafasi ya nne kwenye Ligi msimu uliopita, walianza kampeni ya Ligi msimu huu kwa sare ya goli 2-2 mbele ya Udinese.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares