Juve yaishinda Inter Milan katika Derby ya Italia

62

Ilikuwa mechi kali kwa pande zote mbili na mwishowe ni Juventus iliyofanikiwa kujidai. Bao la kichwa la Mario Mandzukic liliwapa Juve ushindi mwembamba dhidi ya Inter Milan na kupanua uongozi wao wa msimamo wa ligi hadi pointi 11 kabla ya michuano ya Jumamosi.

Mcroatia huyo aliiunganisha kwa kichwa krosi ya Joao Cancelo katika kipindi cha pili baada ya Inter kupoteza nafasi kadhaa nzuri katika mtanange huo wa Ijumaa usiku.

Napoli inaweza kupunguza pengo dhidi ya mabingwa Juve wakati watacheza dhidi ya Frosinone. Timu hiyo ya Carlo Ancelotti ambayo iko katika nafasi ya pili itakabiliana na vijana  wa Frosinone ambao wako katika nafasi ya 19.

Ushindi wa Juve katika Derby dItalia una maana kuwa wameifikia rekodi bora zaidi ya timu kuwa na mwanzo mzuri baada ya mechi 5 katika msimu kwenye ligi tano kuu za Ulaya nchini England, Italia, Uhispania, Ufaransa na Ujerumani. Wamewafikia mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain kwa kuzoa pointi 43 mpaka sasa msimu huu

Inter wanasalia katika nafasi ya tatu kwenye ligi, na pengo la pointi 13 dhidi ya Juve, baada ya mechi ambayo wangeshinda.

Author: Bruce Amani