Juve yashinda, CR7 bado yuwatafuta bao

159

Cristiano Ronaldo aliondoka na ushindi katika mechi yake ya kwanza ya nyumbani wakati Juventus walipopata ushindi wa 2-0 dhidi ya Lazio, mabao yakifungwa na Miralem Pjanic na Mario Mandzukic.

Ronaldo, aliyenunuliwa £99.2m kutoka Real Madrid, hajafunga bao hata moja katika mechi mbili za Serie A walizocheza kufikia sasa. Katika mechi hiyo dhidi ya Lazio, mashabiki waliinua mabango yenye jina lake.

Aligusa mpira mara moja pekee eneo la hatari la wapinzani uwanjani Allianz kipindi cha kwanza, na muda mfupi kabla ya bao la pili la Juve alikuwa amepiga shuti kali lakini likarushwa nje na kipa Thomas Strakosha.

Ronaldo ndiye aliyekuwa amefikiwa na mpira ndani ya eneo la hatari kutoka kwa krosi ya Joao Cancelo lakini akashindwa kuupiga vyema na badala yake ulipodunga na kurejea uwanjani Mandzukic akafunga dakika ya 75.

Author: Bruce Amani