Juve yashinda kibabe kwa Inter Milan na kurejesha njia ya nne bora Serie A

Kikosi cha Juventus kinachonolewa na kiungo mshambuliaji wa zamani klabuni hapo Andrea Pirlo kimevuna alama tatu muhimu kwenye ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Italia na kutengeneza mazingira ya kufuzu kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao 2021/22.
Kwenye mchezo huo ilishuhudiwa timu zote zikimaliza dakika 90 zikiwa pungufu kufuatia wachezaji wawili kuonyeshwa kadi nyekundu katika mazingira tofauti na nyakati tofauti.
Magoli ya Juve yalifungwa na kiraka Juan Cuadrado aliyefunga magoli mawili, moja likiwa na penati pamoja na mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo ingawa kabla ya hapo alikosa penati.
Wakati yale ya Inter Milan yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wa Ubeligiji yalifungwa na Romelu Lukaku kwa njia ya tuta pamoja na lile la kujifunga la mlinzi wa Juventus Giorgio Chiellini.
Upande wa Juve walianza kuwa pungufu dakika ya 55 baada ya Rodrigo Bentancur kufuatia marejeo ya picha za VAR wakati mchezo unaelekea kumalizika, Inter walijikuta pungufu baada ya Marcelo Brozovic kuonyeshwa kadi nyekundu pia.
Matokeo hayo yanaifanya Juve kukwea mpaka nafasi ya nne ingawa wamecheza mechi moja zaidi ya timu iliyo nafasi ya tano Napoli ambayo Leo Jumapili imesafiri mpaka kwa Fiorentina.
Mechi yenye maamuzi kwa Juve ni Jumapili ijayo watakapocheza na Bologna endapo wakishinda basi watakuwa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao bila kujalisha matokeo ya timu nyingine.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares