Juventus hoi kwa Lyon, yalazwa 1 – 0

Mabingwa mara nane mfululizo wa Serie A Juventus wamekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Lyon katika mchezo wa raundi ya kwanza hatua ya 16 bora ya Uefa kwenye mchezo uliopigwa nchini Ufaransa.

Alikuwa ni Lucas Tousart ambaye aliitumia vyema krosi ya Houssem Aouar na kumalizia mpira uliokuwa zao goli pekee katika mchezo huo.

Vinara hao wa Seria A Juventus hawana shida sana na taji la ndani kwa maana ya Ligi hata usajili mkubwa ambao wamekuwa wakiufanya ni kwa ajili ya mashindano makubwa kama Uefa hivyo lazima mkondo wa pili nguvu kubwa itatumika kuhakikisha anashinda na kusonga mbele.

Licha ya kuwa ugenini walicheza vyema na kutawala mpaka umiliki wa mpira lakini walishindwa kutengeneza hata nafasi moja ya wazi jambo lililowawia vigumu Cristiano Ronaldo, Paul Dybala na Juan Cuadrado kufanya majaribio golini, hivyo Juventus walishindwa kupiga shuti hata moja lilolenga goli.

Mtanange wa marejeano utapigwa dimba la Allianz Marchi 17 ambapo vibibi wa Turin vitatakiwa kushinda goli 2 kuendelea

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends