Juventus yaiongozea joto Inter Milan

Juventus imerudi katika njia ya ushindi baada ya kuitandika Verona leo Jumamosi kwenye mchezo wa ligi wa goli 2-1 baada ya sare ya 2-2 wiki iliyopita dhidi ya Atletico Madrid katika Uefa Champions League.
Katika mchezo huo, kiungo wa Wales  Aaron Ramsey ameweza kufunga goli lake la kwanza ndani ya Turin katika mchezo wake wa kwanza akiichezea timu hiyo ndani ya Seria A.
Ramsey, 28, alianza rasmi pale alipoingia kama mchezaji wa akiba kwenye ligi ya mabingwa kabla ya kufunga goli katika mchezo wa leo.
Verona waliweza kuongoza mchezo kunako dakika ya 20 kupitia shuti dogo la Miguel Veloso nje kidogo ya boksi la penati.
Wakati mchezo ukionekana kupoa kwa Juventus chini ya Mauricio Sarri, Mreno Cristiano Ronaldo alifunga goli kwa penati katika kipindi cha pili.
Licha ya ushindi mdogo Marash Kumbulla walimaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya Marash kuonyeshwa kadi nyekundu.
Matokeo mengine Serie A.
Udinese 0-1 Brescia
*Inter vs Milan mechi inaendelea.
Msimamo bado unaonyesha kuwa Inter Milan wanaongoza kwa alama 10 sawa na Juventus huku mchezo ukiwa unaendelea kwa timu hiyo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends