Juventus yaishinda Roma na kuwa bingwa wa msimu wa baridi katika Serie A

61

Juventus ilipambana na kupata pointi tatu kufuatia bao la kichwa la Mario Mandzukic katika kipindi cha kwanza kwa kuizaba Roma 1-0. Ushindi huo umewapa ubingwa wa msimu wa baridi huku ikiwa imesalia mechi mbili kabla ya ligi ya Italia kufika nusu.

Juventus ambao wanaonekana kutowekewa kikomo katika kampeni yao ya kutwaa taji la Serie A kwa mwaka wa nane mfululizo, wana uongozi wa pengo la point inane dhidi ya nambari mbili NAPOLI, ambao waliwazaba Spal 1-0.

Nambari tatu Inter Milan wako nyuma ya Juventus na mwanya wa pointi 16 baada ya kutoka sare ya 1-1 washika mkia Chievo Verona.

Lazio iliibamiza Cagliari 3-1 na kuiruka AC Milan katika nafasi ya nne ambayo ndio tiketi ya mwisho ya Champions League. Lazio sasa iko mbele ya Milan na pengo la pointi moja, baada ya vijana hao wa kocha Gattuso kushindwa 1-0 na Fiorentina.

Author: Bruce Amani