Juventus yajiandaa kuishi bila Ronaldo, ukifika dau unaachiwa

Juventus imemwambia staa wao Mreno Cristiano Ronaldo kuwa iko tayari kumuuza lakini kwa klabu itakayofikia vigezo vyao.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid Ronaldo, 36, amebakiza mwaka mmoja kwenue mkataba wake kuendelea kutumika klabuni hapo.

Hatima ya mshambuliaji huyo imekuwa gizani hasa baada ya kuomba kutoanza kwenye mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A dhidi ya Udinese.

Wakala wa Ronaldo Jorge Mendes amekuwa akizungumza na klabu nyingine Ulaya tangia tetesi hizo kuibuka ambapo Manchester City na Paris St-Germain ni vigogo wapiganio dodo mwembeni.

Inaonyesha Ronaldo anahitaji kuondoka kufuatia klabu hiyo kuonekana si ya ushindani kwani tangia kutua klabuni hapo ameshindwa kuifikisha hatua nzuri za Ligi ya Mabingwa ambapo robo fainali imekuwa kama mafanikio kwa klabu hiyo tangu CR7 aliposajiliwa.

Msimu uliopita, Juventus ilikosa ubingwa wa Ligi ya ndani na kufuta utawala wa misimu takribani tisa, na Inter Milan ambao walikuwa wanaonekana kuwa na kikosi bora na kipana.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares