Juventus yamtimua kocha Andrea Pirlo baada ya msimu mmoja tu

222

Juventus imethibitisha kuwa haitaendelea na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Andrea Pirlo baada ya kuifundisha kwa msimu mmoja tu ndani klabu hiyo ya Serie A.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 42, hakutegemewa kurithi mikoba ya Maurizio Sarii mwishoni mwa msimu uliopita na amekiongoza kikosi chake Juventus kukosa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A kwa mara ya kwanza tangia mwaka 2012.
Vibibi Kizee vya Turin vimemaliza kandanda ya Serie A ikiwa nafasi ya nne na kushuhudia ubingwa ukienda kwa Inter mbele huku wakifuzu siku ya mwisho.
Aliyewai kuwa kocha klabuni hapo, Massimiliano Allegri anatajwa kurithi mikoba yake ikiwa ni mara ya pili katika klabu hiyo.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na klabu ilisema “Asante Andrea. Haya ni maneno ya kwanza ambayo tunaweza kuyasema kwako baada ya muda wa mwaka mmoja kuwa pamoja”.
Pirlo alicheza mechi 164 ndani ya Juventus kuanzia mwaka 2011 mpaka 2015 na ameshinda mataji manne ya Seria A baada ya kujiunga akitokea AC Milan.

Author: Asifiwe Mbembela