Juventus yapeta mbele ya Kyiv, Borrusia Dortmund yatwangwa na Lazio

Michezo mbalimbali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeanza rasmi leo Jumanne kwa msimu mpya wa 2020/21 huku Mabingwa watetezi wa Serie A Juventus wakianza vyema kampeni hizo hata bila kuwepo kwa Cristiano Ronaldo.

Staa wa zamani wa Real Madrid na Chelsea Alvaro Morata alitupia bao mbili katika ushindi huo dhidi ya Dynamo Kviv huku staa wa timu hiyo Ronaldo akikosekana kwenye mchezo huo akiendelea kujitenga mwenyewe kwa siku 14 baada ya kuonekana kuwa na maambukizi ya Covid-19.

Kwa upande mwingine, Borrusia Dortmund imekutana na kipigo cha goli 3-1 dhidi ya timu ngumu ya Lazio katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliochezwa nchini Italia.

Magoli ya Lazio yamefungwa na nahodha wa timu hiyo Ciro Immobile, lile la kujifunga na Marwin Hitz kabla ya mshambuliaji wa Norwei Erling Haaland kutupia goli la kufuatia machozi.

Lazio wakaona haitoshi kushinda mbili moja wakaongeza lingine, Lazio ambao msimu uliopita walikamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Seria A ambapo Jean-Daniel Akpa Akpro aliandikisha goli lingine na la mwisho kwao.

Author: Asifiwe Mbembela