Juventus yazidhibiti Inter na Napoli

58

Juventus ilipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Cagliari Jumamosi na kubaki kileleni mwa Serie A na pengo la pointi sita dhidi ya Inter Milan na Napoli. Mabao ya Juventus yalitiwa kimyani na Paulo Dybala na Juan Cuadrado huku Filip Bradaric akiwapa zawadi kwa kujifunga katika lango lake

Juventus ambayo haijapoteza mchuano wowote mpaka sasa ina pointi 31 baada ya mechi 11, ambapo walipoteza pointi mbili pekee katika sare yao ya 1-1 dhidi ya Genoa,ambao walichabangwa 5-0 na Inter, wakati Napoli waliwabwaga Empoli 5-1 katika mchuano wa Ijumaa. Cagliari wana pointi 13.

Mapema mjini Milan, Inter watamshukuru Roberto Gagliardini aliyefumania nyavu mara mbili katika ushindi wao was aba mfululizo na kukamata nafasi ya pili kwenye msimao wa ligi. Wafungaji wengine walikuwa ni Matteo Politano, Joao Mario na Radja. Sasa Nerazzurri wana pointi 25,  mbele ya Napoli na tofauti ya mabao

Mjini Florence, Fiorentina na Roma zilitoka sare ya 1-1 wakati Jordan Veretout aliwafungia wenyeji penalti katika kipindi cha kwanza naye Alessandro Lorenzi akawasawazishia wageni dakika tano kabla ya mchezo kuisha.

Timu zote mbili zimesonga hadi pointi 16, huku Fiorentina ikiwa mbele katika nafasi ya sita kwa tofauti ya magoli.

Author: Bruce Amani