Kabumbu ya VPL 2020/21 kufikia tamati Jumapili

Ligi Kuu Tanzania Bara inafikia ukomo Leo Jumapili Julai 18 kwa timu zote 18 kushuka dimbani katika viwanja mbalimbali kuwania alama tatu na nyingine kukamilisha ratiba kufuatia kuvuna lengo hitajika kwa msimu wa 202/21.

 

Wakati Ligi ikifikia tamati, bingwa ameshapatikana ambaye ni Simba Sports Club ikiwa ni mara ya nne mfululizo, Simba ambayo itashuka dimbani kumenyana vikali dhidi ya Namungo Fc Jijini Dar es Salaam katika dimba la Benjamin Mkapa. Mechi hiyo pia itatumika kukabidhi ubingwa.

 

Mbali na mchezo huo, mchezo mwingine mkubwa Yanga ambayo imetinga hatua ya fainali ya Kombe la ASFC itacheza dhidi ya Dodoma Jiji dimba la Jamhuri Dodoma.

 

Hata hivyo, kuna michezo yenye kuamua nani wa kushuka nani kucheza hatua ya mtoano (plays offs) na nani kusalia kwenye dakika hizi za lala salama.

 

Mchezo wa KMC dhidi ya Ihefu uwanja wa Uhuru ni muhimu sana kwa Ihefu kushinda huko maombi yakiwa mabaya kwa Coastal Union ambao wanamenyana na Kagera Sugar Mkwakwani Tanga, Tanzania Prisons Vs Gwambina dimba la Nelson Mandela ni mchezo mwingine ambao Ihefu iliwabakie VPL 2021/22 lazima matokeo yawe mabaya kwa Gwambina, pamoja na mchezo wa JKT Tanzania dhidi ya Mtibwa Sugar ni mchezo mwingine ambao ni mgumu wenye hatima ya Ihefu na timu yenyewe ya JKT.

 

Michezo mingine ambayo itapigwa Leo Jumapili ni Ruvu Shooting dhidi ya Azam Fc, na Biashara United ugenini kwa Mbeya City.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares