Kagera Sugar Waichapa Mbeya City

250

Kagera Sugar wamefanikiwa kuvuna ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mtanange uliochezwa uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kwenye mechi ambayo Kagera Sugar wamemaliza wakiwa pungufu kufuatia kadi nyekundu, bao pekee limefungwa na Ally Nassor Iddi dakika ya 87.

Matokeo hayo yanaifanya Kagera Sugar kufikisha pointi 35 na kusogea nafasi ya saba, wakati Mbeya City wanabaki na pointi zao 27 nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 27.

Author: Asifiwe Mbembela