Kagere, Ajibu wakosa penati Simba ikitinga robo fainali FA

64

ikosi cha Simba leo kimetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania kwa ushindi wa penalti 3-2 mbele ya Stand United baada ya sare ya goli 1-1 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa Uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga.

Dakika 90 zilikamilika kwa Stand United kuwa na matokeo ya goli 1-1 huku lile la Simba likifungwa na Hassan Dilunga na la Stand likitiwa kimiani na Miraj Saleh kunako dakika ya 67.

Tamati ya mchezo huo iliruhusu kuanza kwa matuta kupata timu moja itakayoingia robo fainali ambapo penalti upande wa Simba zilifungwa na Clatous Chama, Deo Kanda na Hassan Dilunga huku Meddie Kagere na Ibrarahim Ajibu wakikosa penalti zao.

Aidha, upande wa Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza penati zao zilifungwa na Brown Raphael na Juma Ndaki.

Hiyo ina maanisha Simba imetinga rasmi robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho FA.

Author: Bruce Amani