Kagere, Miquissone kusafiri na Simba Sc kuwafuata Plateau United
Staa wa zamani wa Gor Mahia Meddie Kagere amejumuishwa kwenye kikosi cha Simba SC kinachosafiri leo kuelekea Nigeria kumenyana vikali dhidi ya Plateau United katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbali na Kagere ,winga Lui sMiquissone yuko kikosini pia. Simba SC imetaja jumla ya wachezaji 24 ambao watasafiri kwa ajili ya mchezo wa Novemba 27 siku ya Ijumaa.
Wekundu wa Msimbazi wamepangiwa mabingwa wa Ligi ya Nigeria Plateau kwenye hatua za awali ambapo mkondo wa kwanza utachezwa Nigeria kabla ya ule wa marudiano utakaopigwa dimba la Mkapa Disemba 4. Kwenye kikosi hicho pia amejumuisha Luis Miqussone ambaye hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoshinda goli 7-0 mbele ya Coastal Union Jumamosi sawa na Meddie Kagere. Simba wamethibitisha kuwa timu itaondoka kupitia uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro jioni ya tarehe 24 Novemba kuelekea Ethiopia-Nigeria.
Kikosi cha Simba kwa ujumla wake kiko hivi-:
MAGOLIKIPA:- Aishi Manula, Ally Salim, na Beno Kakolanya.
VIUNGO:- Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Rally Bwalya, Hassan Dilunga, Francis Kahata, and Clatous Chama.Walinzi: Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Ibrahim Ame, Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma.
WASHAMBULIAJI:- John Bocco, Meddie Kagere, Miraji Athumani, Bernard Morrison, Luis Miquissone and Ibrahim Ajibu.