Kai Havertz hana hofu ya kiwango chake, amuamini Lampard

303

Kiungo mshambuliaji ghali wa Chelsea Kai Havertz amesema hana hofu ya kiwango chake kwani haangalii mzigo alionao kwa sababu anataka ajifunze zaidi kutoka kwa kocha Frank Lampard.

Kiungo huyo alijiunga na The Blues akitokea Bayer Leverkusen mwanzoni mwa mwezi Septemba ambapo kabla ajaamua kujiunga na Chelsea mchezaji huyo anayetumia mguu wa kushoto alikuwa anahusishwa kutua Real Madrid.

Katika wachezaji ambao Chelsea imewavuta darajani katika dirisha hili kubwa la usajili, yeye (Kai Havertz, 21) ndiye ghali zaidi ambapo ametumia pauni milioni 71.

“Katika soka la sasa ni jambo la kawaida hela kama hii kutolewa” alisema kinda huyo mwenye miaka 21.

“Haiwezi kunisababiashia hofu yoyote kwa sababu nilikuwa sifanyi vibaya nilikotoka, nadhani ndio maana hata bei yangu ni kubwa”.

Havertz, alicheza mechi yake ya kwanza katika ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Brighton siku ya Jumatatu ambapo anatajwa kama miongoni mwa vijana wenye ubora mkubwa barani Ulaya.

Author: Asifiwe Mbembela