Kamati ya Olimpiki Kenya kutangaza bajeti ya Tokyo 2020

62

Kamati ya Olimpiki nchini NOCK itatangaza bajeti yake ya michezo ya Olimkpiki ya Japan mwaka wa 2020, wiki ijayo baada ya kukutana na mashirikisho kadhaa ya michezo nchini. Naibu rais wa kamati hiyo Waithaka Kioni anadai watajua hali ya mashirikisho yote yaliyofuzu  na yaliosalia na mechi za kufuzu kabla ya kutangaza bajeti hiyo.

Inakisiwa kuwa huenda wakawa na baejti ya zaidi ya wachezaji 100. Wakati wa mashindano ya Olimpiki ya Rio 2016, walikua na wanariadha 89 na  kutumia  shilingi million 530.

Author: Bruce Amani