Kampeni mpya ya kupinga ubaguzi wa rangi yazinduliwa na Man United

Klabu ya Manchester United kupitia kwa kocha wake Ole Gunnar Solskjaer imethibitisha kuwa imezindua kampeni maalumu ya kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi na udhalilishaji kwa wanamichezo.

Man United wametangaza ujio wa kampeni hiyo maalumu Ijumaa Aprili 2

Klabu hiyo ambayo kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL, imepanga kuleta mfumo ambao utakuwa wa utoaji wa taarifa kupitia mitandao ya kijamii juu ya mtu/watu wanaofanya ubaguzi mitandaoni.

“Kampeni hii inaonekana itakuwa na matokeo chanya, wacha tuone” alisema kocha Solskjaer.

United watakuwa wanatumia mechi za nyumbani kutangaza ujumbe wao wa kupinga vitendo hivyo, ambapo mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Brighton siku ya Jumapili.

Siku za karibuni wachezaji mbalimbali wa Manchester United na nje ya United wamekuwa wakikumbana na ubaguzi wa rangi na uzalilishaji, Marcus Rashford, Fred, Axel Tuanzebe, Bukayo Saka, na Lauren James ni baadhi tu ya wachezaji hao.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares