Kane aongeza presha ya kubakia Spurs, njaa ya mataji kumkimbiza

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur Harry Kane amesema umefika wakati anatamani kubeba mataji lakini timu yake imekuwa ikishindwa kufanya hivyo, na karibuni Spurs ilifungwa bao 1-0 Kombe la Carabao.

Kane ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa England hajashinda taji lolote ndani ya Spurs katika umri wa miaka 27, kwenye fainali ya Kombe la Carabao walipoteza kwa Manchester City ikiwa ni fainali ya tatu kupoteza kwa nyakati tofauti.

Strika huyo amesema msimu huu haukuwa upande wao, maana ulikatisha tamaa ambapo klabu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wanaweza kupoteza nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya.

“Nahitaji kushinda mataji makubwa, tunatakiwa kujituma zaidi kupata mataji” alisema Kane ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Real Madrid, Manchester City, PSG na Manchester United.

Mkataba wa sasa wa Harry Kane unakamilika mwishoni mwa mwezi Juni 2024, ambapo amefunga goli 31 ndani ya mechi 44.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares