Kante arudi uwanja wa mazoezi Cobham baada ya kukaa nje kwa muda sababu Corona

Kiungo mkabaji wa Chelsea N’Golo Kante amerudi katika mazoezi ya pekee yake baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda sasa kutokana na hofu ya virusi vya Corona.

Kiungo huyo wa zamani wa Leicester City raia wa Ufaransa alianza mazoezi katika utaratibu uliowekwa na klabu Mei 19 lakini aliamua kusitisha mazoezi hayo maamuzi yaliyoungwa na klabu yake The Blues.

Hata hivyo ameanza rasmi mazoezi katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham.

Kante alisababisha hofu kubwa mwaka 2018 baada ya kuzimia mazoezini. Mwaka huo huo kaka yake alipoteza maisha kwa sababu ya matatizo ya moyo.

Kante na nahodha wa Watford Troy Deeney ndio wachezaji pekee waliokuwa wameweka wazi kutoendelea na mazoezi kutokana na hofu ya Covid-19.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends