Kante, Pulisic fiti Chelsea kuwavaa Porto Ligi ya Mabingwa

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amethibitisha kuwa nyota wake wa kimataifa wa Marekani Christian Pulisic atakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Porto katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali Jumatano Aprili 7.

Mchezaji huyo alitolewa nje ya uwanja katika mchezo ulioisha kwa Chelsea kupigwa goli 5-2 dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi iliyopita kutokana na hofu ya majeruhi lakini sasa Tuchel amesema Pulisic amesafiri na kikosi kwenda Hispania.

Kiungo mkabaji wa zamani wa Leicester City N’Golo Kante naye pia yuko fiti kwa ajili ya mechi hiyo baada kuumia.

Washambuliaji Tammy Abraham na Olivier Giroud wote wamesafiri na timu, ili kuongeza nguvu kufuatia kupoteza mechi ya Ligi wikiendi iliyopita.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares