KCCA yatinga fainali ya Kombe la CECAFA

Kinda wa Uganda Allan Okello amefanikiwa kuifikisha fainali klabu ya KCCA baada ya kufunga goli 2 katika ushindi wa goli 4-3 katika muda wa ziada baada ya sare ya 2-2 kwenye muda wa kawaida dhidi ya Green Eagles ya Zambia nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Kagame.
Okello alifunga goli la kuongoza kwa klabu yake kabla ya kufunga goli la pili kuelekea kukamilika kwa dakika 90, goli lililopelekea dakika 120 kuongezwa.
Magoli ya Green yamefungwa Amity Shamende, Sadat Anaku baada ya makosa ya kiulinzi, na Mukabanga Siambombe.
Licha ya Green Eagles kujitutumia Christopher Chola alikuja kukatisha ndoto zao baada ya kufunga goli la ushindi na kufanya matokeo kuwa 4-3.
KCCA itakutana na klabu kati ya Azam au AS Maniema hatua ya fainali.
Fainali itafanyika siku ya Jumapili.
KCCA v Azam/AS Maniema
Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu itafanyika mapema.
Green Eagles v Azam/AS Maniema

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends