Kelvin John Kutua Genk kwa Samatta

476
Kinda wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kelvin John usiku wa Jana Alhamisi amesafiri kuelekea nchini Ubelgiji, kufuata mualiko wa klabu ya Genk anayochezea mtanzania Mbwana Ally Samatta.
Kelvin (16) alitumiwa mualiko na klabu hiyo yenye timu yake inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza nchini humo Julai 25 mwaka huu.
Kwa mujibu wa mualiko huo,umeeleza kuwa kinda huyo wa Taifa stars na Serengeti Boys atasaini mkataba na makubaliano mwezi huu wa Septemba.
Mualiko huo ulieleza kuwa gharama za Safari ikiwemo malazi,chakula na bima vitagharamiwa na klabu ya Genk.
Kelvin ni miongoni mwa wachezaji vijana wenye ushawishi wa soka kwa sasa nchini, hali iliyosababisha kujumuishwa katika kikosi cha wachezaji walioitwa na aliyekuwa Kocha wa Taifa stars Emmanuel Amunike katika michuano ya Fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) mwezi juni 2019 na baadae alitolewa kupata idadi ya wachezaji 23 wa timu ya Tanzania.

Author: Bruce Amani