Kenya yakabwa na Togo, Coromos yagawana pointi na Misri

245

Misri wamekabwa kwa sare ya pili mfululizo kwenye mechi za kufuzu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2021 baada ya wenyeji Comoros wakiongozwa na nahodha Jimmy Abdou kupambana na kutoka sare tasa.

Baada ya sare yao ya 1 – 1 na Kenya ALhamisi wiki iliyopita katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi G, Misri walikamata pointi moja mjini Moroni. Kulikuwa na matokeo ya sare katika mtanange mwingine wa Kundi G mjini Nairobi wakati Kenya ikitoka sare ya 1 – 1 na Togo. Johanna Omolo anayecheza kandanda lake nchini Ubelgiji aliipa Harambee Stars bao la uongozi kabla ya Malcolm Barcola kusawazisha kupitia kichwa katika kipindi cha pili.

Matokeo hayo hayo yana maana kuwa Comoros sasa wanaongoza kundi hilo na pointi nne kutokana na mechi mbili, Misri na Kenya zina pointi mbili huku Togo ikiwa na pointi moja.

Matokeo ya Afcon 2021:

Jumatatu:

  • Sao Tome and Principe 0-1 Ghana (Group C)
  • The Gambia 2-2 DR Congo (Group D)
  • Cape Verde 2-2 Mozambique (Group F)
  • Comoros 0-0 Egypt (Group G)
  • Kenya 1-1 Togo (Group G)
  • Botswana v Algeria (Group H)

Author: Bruce Amani