Kenya yaunga mkono kupigwa marufuku wanariadha wake

150

Shirika linalopambana na utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu mwilini nchini Kenya, limeunga mkono hatua iliyochukuliwa ya kuwapiga marufuku wanaraidha wawili nchini humo.

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika hilo, Japhter Rugut, amesema kuwa shirika lake limechukua hatua hiyo baada ya matokeo kubainisha kuwa wanaridha hao walitumia dawa hizo.

Rugut alisema kuwa alliyekuwa mshindi wa mbio za mita elfu kumi katika mashindano ya Jumuiya ya Madola, Joyce Chepkirui, na mwanariadha wa masafa marefu, John Jacob Kibet Kendagor, walipatikana na hatia hiyo kwenye mashindano yaliyofanyika nje ya nchi.

Mapema Rais wa Riadha nchini Kenya, Jackson Tuwei, alikuwa amewaonya wanariadha dhidi ya kujihusisha na ulaji moku akisema kuwa watakaopatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria. Tuwei ameongeza kusema kuwa dawa hizo hazisambaratishi tu mchezo wa huo wa riadha lakini pia zinaharibu jina zuri la taifa la Kenya kwenye medani ya kimataifa.

Author: Bruce Amani