Kesi ya Morrison CAS yamalizika, yasubiriwa maamuzi

Klabu ya Yanga kupitia akaunti zao za mitandao ya kiyjamii Leo Alhamis Julai 29, 2021 imethibitisha kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi Michezoni CAS imemaliza kulisikiliza kesi ya rufaa ya Klabu ya Yanga dhidi ya mchezaji Bernard Morrison.

Yanga imesema mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, CAS itatoa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zake kuanzia sasa mpaka Agosti 24, 2021.

Kupitia taarifa hiyo, klabu ya Yanga imewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwa wavumilivu katika kuhakikisha wanapata haki yao.

“Uongozi wa Yanga unawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki kuwa na subira, wakati huu ambapo Mahakama hiyo inaendelea kukamilisha uamuzi wake” wameandika Yanga

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares