Kibu Denis, Kisubi watua Simba kimya kimya

Jeremiah Kisubi na Kibu Denis wameonekana wakifanya mazoezi na kikosi cha Simba chini ya kocha Didier Gomes Da Rosa katika mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kuanza kwa mazoezi hayo kunaashiria kuwa wamekamilisha usajili ingawa umekuwa wa kimya kimya tofauti na ilivyokuwa kwa wachezaji wengine kama Peter Banda, wanajiunga na Simba baada ya wachezaji wengine kutokea Morocco.

Kibu aliyekuwa anakipiga kunako klabu ya Mbeya City ilielezwa kuwa amekamilisha kujiunga na Simba lakini hakutambulishwa sawa na Kisubi ambaye ni mlinda mlango aliyekuwa anachezea klabu ya Tanzania Prisons.

Wachezaji waliokuwepo kwenye mazoezi ni Jonas Mkude, Beno Kakolanya, Ally Salim, Hassan Dilunga, Cris Mugalu, Jimson Mwanuke, Lary Bwalya na Gadiel Michael.

Wengine ni Kibu Denis, Ibrahim Ajibu, Pascal Wawa, Hassan Dilunga, Henock Inonga, Kennedy Juma, Benard Morrison, Sadio Kanoute, Joash Onyango, Abdulsamad Kassim, Pape Sakho na Duncan Nyoni

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares