Kichapo cha Napoli kimeisogeza Juventus karibu na taji

Je, mshindi wa ligi kuu ya Italia atajulikana wikiendi hii? Nambari mbili kwenye ligi Napoli wamepata kipigo cha kushangaza cha 2 – 1 dhidi ya timu ya upande wa mkia wa ligi Empoli ambao wametoka katika eneo la kushushwa ngazi.

Vijana wa Ancelotti, Napoli wako nyuma ya vinara Juventus na mwanya wa pointi 18 huku zikiwa zimesalia mechi nane msimu kukamilika.

Taji huenda likaamuliwa wikiendi hii kama Juve itailaza AC Milan Jumamosi na Napoli ishindwe na Genoa siku itakayofuata.

 

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends