Kikosi Bora Msimu 2020/21 EPL chatawaliwa na Manchester City

Kikosi bora cha Ligi Kuu England kimetolewa rasmi huku kikiwa na wachezaji sita wa Manchester City, mchezaji mmoja pekee akijitokeza kwa mara ya pili mfululizo Kevin de Bruyne.
Mchezaji aliyeingia upande wa kulia ni Joao Cancelo, kushoto ni beki wa Manchester United Luke Shaw, katikati ni John Stones na Ruben Dias wote Man City, Ilkay Gundogan na Kevin de Bruyne (Man City) pamoja na Bruno Fernandes wakicheza shimoni.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Misri Mohammed Salah akiwa na bao 22, Harry Kane bao 23 na Heung-Min Son wakimalizia eneo la mwisho.
Nafasi ya mlinda mlango imeenda kwa kipa wa Manchester City Ederson ambaye goli lake halijaguswa katika mechi 19 akiandikisha rekodi mpya.
Licha ya kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kufika fainali ya Kombe la FA kisha kupoteza kwa Leicester City klabu ya Chelsea haijaingiza mchezaji yeyote.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares