Kikosi cha Shujaa cha ubingwa wa Afrika chatangazwa

Mkurugenzi wa kiufundi wa Muungano wa Raga nchini Kenya Paul Feeney amekitaja kikosi cha wachezaji 12  cha Shujaa  cha mechi za ubingwa wa Afrika kwa raga ya wachezaji saba kila upande ambazo pia zitatumiwa kama mechi za kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki jijini Tokyo mwaka wa 2020. Mashindano hayo yataanza Ijumaa tarehe nane na Jumamosi  tarehe tisa mwezi huu jijini Johannesburg Afrika Kusini.

Mashindano hayo yatazishirikisha timu 14  ambazo zimeorodheshwa  kwa mujibu wa matokeo ya ya mwaka jana .kenya ni ya pili baada ya kushindwa na zimbabwe  katika fainali iliyofanyika Tunisia .Timu nyingine ni  Uganda, Madagascar, Zambia, Tunisia, Senegal, Morocco, Namibia, Ghana, Botswana, Mauritius, Ivory Coast na  Nigeria.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends