Kikosi cha Simba kinachovaana na Nkana ya Zambia

Simba Sports Club inashuka uwanjani Jumamosi hii kucheza dhidi ya Nkana FC ya Zambia katika mashindano ya klabu bingwa Afrika ikiwa ni hatua ya mwisho, mchezo huo utakafanyika katika uwanja Kitwe kuanzia saa 10:30 jioni.
Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kuinyuka Mbabane Swallows goli 8-1.
Timu yoyote itakayoibuka na ushindi katika michezo miwili itasonga mbele kuingia katika hatua ya makundi na itakayoshindwa itaangukia kwenye kombe la shirikisho Afrika.
Kuelekea mtanange huo, Kocha Patrick Aussem amekiweka bayana kikosi chake kitakachoanza dhidi ya Nkana
1.Aishi Manula.
2. Niclolaus Gyna
3.Mohammed Hussein Junior
4.Erasto Nyoni.
5. Pascal Wawa
6. Jonas Gerrard Mkude
7. James Kotei
8. Clatous Chama
9. John Raphael Bocco
10. Meddie Kagere
11. Emmanuel Okwi
Simba pamoja na kutoshiriki kwa misimu kadhaa bado ina historia nzuri ya kufanya vizuri katika mashindano ya CAF.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares