kikosi dhaifu cha Barca chapewa kipigo na Celta Vigo

Mabingwa wapya wa La Liga Barcelona wamepata kipigo cha kushangaza dhidi ya Celta Vigo baada ya kuwapumzisha Lionel Messi, Luis Suarez na Gerard Pique.

Maxi Gomez alifungua ukurasa wa mabao kwa upande wa Celta baada ya bao lao kufutwa na mfumo wa VAR

VAR baadaye ikawapa Celta penalty na Iago Aspas akasukuma wavuni kufanya mambo kuwa 2 – 0.

Timu hiyo ya kocha Ernesto Valverde pia ilikosa huduma za Ivan Rakitic, Sergio Busquets na Jordi Alba – na pia ikampoteza Ousmane Dembele baada ya kuumia mapema.

Author: Bruce Amani